Home || The Aggressive Vision || Prophetic Word Of The Lord || On Line Library || Current Articles and What's New
Free Literature || Visions from The Lord || More About ACMTC || Contact


Mwanadamu Ni Lazima Afanye Nini Ili Aokolewe

(What Man Must Do to

Be Saved)

HATUWEZI KUSHUGHULIKA na swali la muhimu zaidi ya hili. Furaha na amani katika maisha haya na umilele ujao inategemea ujuzi wa jibu sahihi la swali hili –“ Yanipasa nifanye nini ili nipate kuokolewa?’’ Jibu hili laweza lisiwe rahisi kama baadhi wanavyoonekana kufikiri. Tumezungukia mafundisho yote ya Agano Jipya ili kugundua sehemu ya Mungu katika wokovu wetu ni ipi, kwa hiyo inaonekana wazi kuwa TUNGETAFITI KATIKA AGANO JIPYA vilevile ili tugundue sehemu ya mwanadamu katika wokovu wake mwenyewe ilivyo.

    Kwa ajili ya haki na uadilifu hatuyafungii mawazo yetu kwenye kipengele kimoja au vichache kwenye maandiko haya mengi lakini tunaonesha kila andiko linaloonesha hitaji la wokovu wetu. Kama mtu angepitia Agano Jipya na kufanya kila andiko linalomwambia chakufanya kwa ajili ya yeye kuokolewa, tunaamini angekuwa na orodha kama hii tunayoitoa hapa chini.

Sehemu ya mwanadamu kwa ajili ya wokovu wake mwenyewe:

1.  Ni lazima alisikie Neno (Yoh 5:24; 10:27; Mdo 18:8; Rum. 10:17).

2.  Ni lazima atubu (Luke 13:3-5; Mdo 3:19; 26:20).

3.  Ni lazima ageuke (Mat. 18:3, American Standard Version [ASV]).

4.  Ni lazima aamini (Yoh 1:12; 3:15-18).

5.  N lazima ampokee Kristo (Yoh 1:12).

6.  Lazima aje kwa Kristo (Yoh 6:37; Mat. 11:28-30).

7.  Ni lazima aule mwili wa Kristo na kuinywa Damu Yake (Yoh 6:53-57).

8.  Ni lazima anywe maji ya uzima (Yoh 4:13, 14).

9.  Ni lazima amwone Mwana na kuamini katika Yeye (Yoh 6:40).

10.Ni lazima aingie katika mlango ambao ni Kristo (Yoh 10:9).

11.Lazima amkiri Kristo (Mat. 10:32-33; Rum. 10:9, 10).

12.Ni lazima abatizwe au aamini na kubatizwa au atubu na kubatizwa (Mark 16:16; Yoh 3:5; Mdo 2:38; 22:16).

13.Ni lazima ashike amri (Mat. 19:17; Luk 10:25-29; Gal. 3:12).

14.Ni lazima atii (Yoh 3:36, ASV; 2 The. 1:8).

15.Ni lazima ayafanye mapenzi ya Baba wa Mbinguni (Matt. 7:21; 1 Yoh 2:17).

16.Ni lazima avumilie hadi mwisho (Matt. 24:13; Yoh 8:31; Kol. 1:23; Ebr. 4:1).

17.Ni lazima aombe (Rum. 10:13; Luk 18:13-24; Luk 23:42; Mdo 2:21).

18.Ni lazima amfuate Yesu Kristo (Yoh 8:12; 10:27; Mat. 8:22).

19.Ni lazima awasamehe watu (Mat. 6:14-15; Mark 11:25, 26)

20.Ni lazima ajitahidi kuingia kwenye mlango uliosonga na njia nyembamba (Matt. 7:13; Luk 13:24).

21.Ni lazima ayaache yote amfuate Yesu (Luk 14:33; Matt.19:21; 19:29).

22.Ni lazima awachukie ndugu zake naam na nafsi yake mwenyewe kwa ajili ya Yesu Kristo (Luk 14:26; Matt. 10:37).

23.Ni lazima aubebe msalaba wake na kumfuata Yesu (Luk 14:27; Mat 16:24).

24.Ni lazima ayashike maneno ya Kristo (Mat. 7:24-27; Yoh 8:51).

25.Ni lazima awe na huruma na awe anasaidia maskini, waliofungwa na wahitaji (Matt. 25:35-46; Yak. 2:14-17; 1 Yoh 3:17).

26.Ni lazima amwogope Mungu na kuishi kwa haki (Mdo 10:35).

    Tunaamini kwamba kauli hizi zinajumuisha kila hitaji la wokovu ambalo kila msomaji aliyefunguka mawazo anaweza kuliona. Mahitaji haya ya wokovu yakichanganywa pamoja yanafanya njia iliyo ngumu na yenye mchanganyiko wa vingi, lakini tumejaribu kuwa waungwana kwa KUJUMUISHA HALI ZOTE ZA WOKOVU ZILIZOONEKANA KUTUMIKA KATIKA AGANO JIPYA.

    Tuseme nini juu ya mahitaji yaliyo mengi? Hatutamani kupunguza thamani hata chembe ya yale Mungu anayotaka kwa kuyarahisisha, lakini hatuwezi kuhimili kuchanganywa mawazo katika hatua hii. Njia ya wokovu imefundishwa katika namna nyingi na kuwekwa kwenye kauli za namna nyingi katika Agano Jipya, ili kwamba watu wote waifahamu,hata hivyo ni kauli rahisi katika asili yake. Mengi ya mahitaji hayo hapo juu kwa wepesi ni kusema kitu kilekile kwa namna tofauti, lakini kila moja ikiwa na wazo la imani, utayari wa kutumika, kumtegemea, kupokelewa na kufaa. Yote yanaongezea kwenye wazo la imani iokoayo. Mengine ya mahitaji hayo hapo juu sio taratibu za kupata wokovu badala yake ni taratibu za uanafunzi yaani njia ya kumfuata Yesu na kuishi maisha ya Kikristo. Kwa makundi hayo tutayatenganisha kumkiri Kristo, kubatizwa, kutii, kuvumilia hadi mwisho, kuomba, kuwasamehe watu, kupambana, kuyaacha yote, mtu kuwachukia ndugu zake, kuwa na huruma na kuwasaidia maskini.

    Neno moja “amini” ni la muhimu sana kwamba linajumuisha na kufunika vipengele vingine VYOTE vilivyo muhimu kwa wokovu. Wakati mdhambi anapomwamini Kristo, kwa mantiki ya wokovu, anafanya zaidi ya kuamini kwamba; Kristo ndiye, kwamba alifanya upatanisho, kwamba anauwezo wa kuokoa, na kwamba ana shauku ya kuokoa. Anaamni kwa kiwango cha kujiaminisha kwa moyo wote kwa Kristo, kwa sasa na milele, kwa kuafikiana na Kristo na yote yale aliyofanya akiwa ndiye TUMAINI PEKEE, la kubadilisha maisha yake yote ya mfananie Kriso maisha yote. Hii inajumuisha toba, mtu binafsi kuyafuta yale mabaya aliyotamka, kusadiki, kujitoa, ukiri na uadilifu.

Kumtumikia Kristo

    Tunapozungumzia kumwamini Kristo ili kuupata wokovu, tunaweza kupata swali. “Kristo gani [yupi]?” maoni mengi juu ya Kristo yametapakaa siku za leo kiasi kwamba tunatakiwa kuwa makini kwamba mwenye dhambi anamwamini Bwana Yesu Kristo wa Agano Jipya. Hakuna yeyote anayeweza kumwamini Kristo mwingine kuliko yule anayemfahamu kwenye mawazo yake. Wengi picha ya Kristo waliyoikumbatia kwenye fahamu zao wameipata kutoka vyanzo vingine mbali na Agano Jipya, au wamechukua kweli chache za Agano Jipya zinazomhusu Kristo lakini hawakuzichukua zote. Kristo wa Agano Jipya ndiye KRISTO MKAMILIFU wa Biblia nzima! Yeye ni wa milele, wa dunia nzima, yupo kila mahali, mwenye kudra zote, aliyepo kila wakati, asiye na dhambi, aliyejaa neema, Mkombozi aliye Mwanadamu-Mungu, aliyeinuliwa juu ya majina yote yanayoitwa mbinguni juu na chini duniani. Awezaye kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa Yeye. (Ebr. 7:25).

    Kristo wa Agano Jipya sio Kristo wa kisasa: anaye vumilia dhambi, sio Kristo wa Roman katoliki, ambao, ingawaje maalum wana mtazamo wa miundo ya kiothodoksi, busara yao imezidi kwa Bikira Maria, ambapo nguvu za Kristo za ukombozi ziko kwenye sakramenti za kanisa kana kwamba ndiko anakopitia, zimefishwa kwenye mila, desturi, sherehe, na imani zisizo sahihi. Wala sio Mungu wa universal wanaosema tunahitaji kuiga tabia ya Bwana ili tuokolewe na kwamba baadaye atawaokoa wote. Sio Kristo wa Wakristo Sayansi: mzaliwa wa Maria mwenye haki mshirika na Mungu, wazo la kiroho, asiyeathiriwa na hisia za mtu binafsi, asiye na mwili, aliyetofauti na wa dunia, mwenye mwili Yesu.

    Sio Kristo wa Mashahidi wa Yehova, ambaye ni kiumbe aliyeumbwa, mkuu kuliko Malaika lakini mdogo kuliko Mungu. Sio Yesu wa spiritualism; ni mwanadamu tu na yuko katika hali ya kiroho ambalo ni agizo kutoka mahali pa juu, sio Mungu katika mwili. Sio Kristo wa Wamormon (Watakatifu wa Siku za Mwisho): mwana wa Adamu-Mungu na Maria, ambaye hakuzaliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Ambaye anaweza kuokoa tu kwa kupitia kanisa la mormon na ubatizo wa kanisa hilo. Sio Kristo wa Wazo Jipya, Umoja, na wengineo ambao hudai kumjua, hutumia jina lake, wanamchukulia kuwa wa kipekee, lakini wanashindwa kumtukuza na kumwinua juu kama Mungu halisi aliye Mungu halisi, nafsi ya pili katika Utatu wa Mungu.

    Kristo wa Agano Jipya ndio kitu halisi kilicho maalum kwa imani iokoayo. Ni nafsi ya pili ya Ukuu wa Mungu, (Mat. 3:16-17; 28:18-20; Yoh 1:1-3, 2 Kor. 13:14), milele mwana wa Mungu, hajawahi kuumbwa, aliye sawa na Yehova wa Agano la Kale, mmiliki wa kila kilicho cha Mungu lakini aliyejitolea kwa hiari kuzaliwa katika mwili wa kibinadamu na kwa wakati wa kuishi kwake duniani aliweka kando matumizi (sio haki ya umiliki) ya baadhi ya ukuu wake wa ki Mungu, (Flp. 2:5-8), Yeye ni Mungu na Yeye ni mwanadamu, ana asili zote mbili, kamilifu na zote, kwa uhakika ameungamanishwa katika Ubinadamu wa Uungu, Mkombozi (Ebr. 2:9-18). Alizaliwa na bikira bila baba wa kibinadamu (Matt. 2, 3; Luk 1, 2); Hakuwa na dhambi, Mtakatifu, asiye na madhara, asiye najisiwa (Ebr. 7:26, 27); Alifanya miujiza yote aliyopaswa kufanya, alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi za wengine (1Kor. 15:3), alimaliza tatizo la dhambi mara moja kwa wote, akafanya wokovu upatikane kwa njia ya imani peke yake (Rum. 3:21-31; Efe. 2:8, 9); alifufuka toka kwa wafu akawa kwenye mwili wake uliosulibiwa (Luk. 24; Yoh. 20; 1Kor. 15) kwa udhihirisho usiopingika akajionyesha hai (Mdo 1:3); alipaa mbinguni akiwa na mwili uleule uliosulubiwa lakini uliobadilishwa, mwili uliofufuka (Luk 24:50-52; Mdo 1:10, 11), mahali ambapo ameketi sasa mkono wa kuume wa Mkuu aketiye mahali pa juu (Ebr. 1:3), kama Kuhani wetu Mkuu (Ebr. 4:14-16; 7:24-28), mpatanishi (1 Yoh 2:1). Atarudi duniani kwa wakati uliopangwa (Mdo 1:11), kuwapokea walio wake (1 Thes. 4:16-18). Huyu ndiye Kristo wa Agano Jipya. Yeye PEKEE, ndiye awezaye kuokoa.

    Hatumaanishi kuchukulia kwamba kila ambaye hajaokoka anatakiwa kuyajua yote hayo kuhusu Kristo ndipo aokolewe naye. Labda ni watu wachache sana kati ya waliookoka waliwahi kuwa na mtazamo mkamilifu kuhusu Kristo kabla ya kumpokea kama Bwana na Mwokozi wao. Lakini mtu ambaye hajaokoka hatakiwi kuwa na namna yoyote ya kutokuamini kwenye nyanja kuu za ubinadamu wa Kristo na kazi zake kiasi cha kushindwa kujinyenyekeza chini ya Ubwana na Uokozi wa Kristo. ANATAKIWA KUWA TAYARI KUMCHUKUA YESU KRISTO SAWASAWA NA YALE YOTE ANAYOYAFAHAMU KWA WAKATI HUO, NA BAADAYE KUWA TAYARI KUMFUATA KWA JINSI ANAVYOFAHAMU ZAIDI KUHUSU YEYE. Yesu Kristo ataongeza sura yake na kufahamika zaidi na zaidi kwa kila mwanafunzi aliye mtiifu.

Tunawezaje kumshuhudia Kristo kwa waliopotea?

    Kwa kuwa haiwezekani kumweleza mtu aliyepotea kweli zote hizo nyingi kuhusu Nafsi ya Kristo na kazi zake za wokovu, tunapaswa kujiuliza “Tumweleze nini basi? Ni kweli na mambo gani muhimu? Ni kweli gani muhimu kwa uchache kumhusu Yesu Kristo ziwezazo kumwokoa mdhambi aliye potea?”

    Mshuhudiaji ni lazima aweze kuwasilisha kweli nyingi iwezekanavyo kumhusu Kristo, sio kweli kidogo tu kama alizo nazo mwenyewe. Kila kweli inayomhusu Kristo ina nguvu. Ni hatari sana kushikilia kwamba kipengele kimoja tu cha kazi ya wokovu ya Kristo ndicho pekee chenye uwezo wa kuleta neema ya wokovu kwa aliyepotea. KAZI YA KRISTO YA WOKOVU NI UKAMILIFU. Hatuwezi kutenganisha maisha aliyoishi bila dhambi na kujitoa kwake hadi kumwagika damu, wala kumwagika damu na ufufuko wake, wala ufufuko wake na kupaa kwake, wala kupaa kwake na utukufu pamoja na kazi ya Ukuhani mkuu alionao Mbinguni wala kazi yake ya maombezi aliyonayo mbinguni uitenganishe na kurudi kwake mara ya pili, wala kurudi kwake mara ya pili kutoka kwenye kumiliki na kutawala wala mojawapo ya kweli hizi kutoka kwenye uungu wake na utawala wake wa milele. Tunaweza kuanza na kweli yoyote katika hizi na kuongeza mara hadi kufikia kiwango cha kumwonyesha njia ya wokovu. Hata hivvyo mwandishi huyu anaamini kweli moja inayomhusu Kristo inajumuisha yote na yote muhimu na hiyo ndiyo kweli ya Ubwana wake.

    Kwamba tunatakiwa kufafanua kwa shauku ukweli wa ubwana wa Kristo sio jambo la kutilia mashaka. Mfumo huu wa Agano Jipya una uhakikisho. Yesu alifundisha kweli hizi kwa vielelezo akiwa na tamko chanya (Matt. 11:27-30; 16:13-19, 27, 28; Yoh.13:13-16). Petro alisisitiza kuhusu ubwana wa Kristo katika mahubiri yake ya siku ya Pentekoste (Mdo 2:36). Aliirudia tena na tena mbele ya wakuu na watawala wa Israel (Mdo. 4:12). Stefano alikazia kusema kwamba alimwona Yesu mbinguni akiwa Bwana na akazungumza naye kama vile katika maombi yake ya mwisho wakati anakufa. (Mdo. 7:55-59).

    Wakati yule mtesaji Sauli wa Tarso alipotupwa chini kwa ule mwanga uliotoka Mbinguni, alipokuwa njiani kwenda Dameski, alifahamu ya kwamba yule aliyekuwa akinena naye kutoka katika mwanga ule alikuwa Bwana ambaye alitokea katika utukufu wa Shekina katika nyakati za Agano la Kale (Mdo 9:5). Wakati alipojitambua mwenyewe kwa kumlingana Yesu, Paulo alifahamu kuwa Yesu ni Bwana na akajiachilia kwake mara moja na muda wote akawa akisema “Yanipasa kufanya nini Bwana?” (Mdo. 22:10). Paulo na Sila walimhubiri Yesu kuwa ni Bwana kwa wafungwa wa Filipi (Mdo. 16:31). Paulo alisisitiza umuhimu wa kuukiri Ubwana wa Yesu Kristo na kuamini moyoni kwamba alifufuka katika wafu (Rum. 10:9, 10) ili kuokoka. Viumbe vyote ni lazima siku moja, vimkiri Kristo kuwa ni Bwana (Filp. 2:9-11). na, kama wakikiri hivi kwa hiari yao iliyoambatana na imani ya kweli katika maisha haya ya sasa wataokoka. Kama kwa ukweli tukiamini katika ubwana wa Yesu Kristo, tutafanya zaidi ya kumwita “Bwana” tutayafanya mapenzi ya Baba wa Mbinguni (Matt. 7:21-23).

    Ufufuko wa Kristo ulikuwa udhihirisho wa wazi wa u-Bwana wake na u-Mesia wake (Mdo. 2; 1 Kor. 15), na ukweli huu ulikuwa ndio ufunguo mkuu wa mahubiri ya Mitume. Ubwana wa Yesu Kristo ina maanisha ukuu wake wote, na mtawala mkuu asiye na mwisho nyakati zote na kila mahali. Yeye ndiye mwanzilishi wa uzima na hatima ya mtu kwa kuwa anavyo vitu vyote mkononi mwake. Kwake kila mtu atatoa hesabu yake. Wakati mwenye dhambi mpotevu anapotambua maana ya u-Bwana wa Kristo, yeye kama alivyofanya Paulo wa Tarshishi, anakuwa na UTAYARI wa kufanya lolote analoamriwa. Atamwamini Yeye, atampokea, atamfuata na kumtumikia Yeye.

Dk. G. Campbell Morgan anaamini kwamba msisitizo wa kwanza katika mahubiri ya kiinjilisti unatakiwa kuwa Ubwana wa Yesu Kristo. Aliandika;

U-bwana wa Yesu kwanza. Sasa, waweza kuniuliza, ‘lakini haya umeyaweka kwenye mpangilio sahihi? Sio sahihi kwamba jukumu la kwanza la mwinjilisti ni kuuhubiri msalaba wa Kristo? Sifikirii hivyo. Ninaamini ya kwamba jukumu la kwanza la mwinjilisti ni lile la kuwatangazia watu u-bwana wa Kristo…Lakini panaweza kuwepo pingamizi, hawezi kuwa Bwana wa mtu hadi pale huyo mtu atakapookoka. Sahihi kabisa, lakini kwa walio wengi hawawezi kuanza kusikia hitaji hadi pale watakapoletwa mahali pa nuru ya kuukiri u-Bwana wake na kwa hiyo, nasisitiza hili liwe la kwanza. Hii ndio kanuni waliotumia mitume’. ("Evangelism," p. 14).

Mwanadamu anamhitaji Bwana Mwenyenzi, ambaye anaweza kuokoa, kutunza, kulinda, kutoa na kuwapeleka salama Mbinguni. Kristo ni Bwana wa namna hiyo. Tunahitaji kuwaelezea jinsi Kristo alivyokufa msalabani kwa ajili ya dhambi zao, jinsi alivyowalipia deni, jinsi alivyowapatia msamaha wa bure tena mkamilifu. Lakini tunahitaji kuwasisitizia kwamba akiwa kama Bwana, KRISTO ATAWAWAJIBISHA KWA NAMNA WALIVYOICHUKULIA SADAKA YAKE ALIYOTOA YA WOKOVU, na kwamba anatakiwa kupokelewa kama Bwana na Mwokozi. Labda baadhi ya uinjilisti wetu umekuwa dhaifu sana pia usio imara kwa kuwa mkazo wote tumeuweka kwenye wokovu wa Kristo bila kuzungumzia Ubwana wake.


Kwa maelezo zaidi kuhusu ACMTC TANZANIA, au jinsi utakavyoweza kujihusisha, wasiliana na Meja Frank & Elina Materu: S.L.P. 7579 Dar es Salaam, Tanzania. Barua pepe: materufrank@yahoo.com